
Na Busara Ziro| GAZETI LA AMANI| BUSARA ZIRO
SHIKAMOO babu, mimi naitwa Mwajuma wa Morogoro. Tatizo langu babu, mume wangu ananuka sana mdomo na akivua viatu ndani hakukaliki.
Nimejaribu kumueleza lakini haisaidii, imefika hatua hata ukifika muda wa kupeana haki yetu ya ndoa, napata kero kubwa kwani nasikia harufu mbaya sana ya mdomo wake. Nisaidie nifanyeje?
JIBU: Hilo tatizo kitaalamu linaitwa smell, inawezekana mumeo anakunywa pombe za kienyeji almaarufu mataputapu na kula vitu vilivyooza. Ushauri wangu, akiingia tu ndani, ziba pua zako kwa kutumia mikono, pamba au unaweza kununua vile vitambaa maalum vya kuziba pua. Pia akivua viatu vyake na soksi, nenda kavitupe nje. Pia kwenye suala la haki ya ndoa, kuanzia leo mnyime, hafai kabisa huyo, njoo kwangu mimi napiga mswaki mara tatu kwa siku, nanukia marashi kila sehemu. Ntakupigia usiku.