
Rais John Magufuli, amesema watapitia upya na kuchambua uongozi wa Benki ya Wanawake nchini (TWB), ili benki hiyo iweze kufanya kazi kiushindani.
Rais Magufuli amesema hayo leo Desemba 8, mjini Dodoma wakati akizindua mkutano wa tisa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kuongeza kuwa benki hiyo imekuwa ikimkandamiza mwanamke hasa katika mikopo kwa kulipia riba kubwa na wakati huo huo wanufaika wengi wa mikopo hiyo ni wanaume.
VIDEO: HOTUBA YA RAIS MAGUFULI
Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli ameutaka uongozi mpya atakaouchagua kumsaidia kufanya mabadiliko katika benki hiyo ili ifanye kazi kwa ufanisi na ushindani.
“Kumekuwa na kawaida kuwa benki hii kila anapokuwa mwanamke haifanyi vizuri badala yake imekuwa ya kuwanyonya wanawake, nimesema haya na ni matumaini yangu mmenielewa,” amesema.