×

Malick; Msomi, Msanii Mwenye Matukio Ya Kusikitisha!

Q Jay (kulia) akiwa na D Malick.

ABDULMALICK Simbamgeni ni jina kubwa ukizungumzia miongoni mwa wasomi wanaofanya Muziki wa Bongo Fleva akitambulika pia kwa jina la kisanii la D. Malick.

Katika kumbukumbu za kawaida, D. Malick ndiye msanii, msomi pekee mwenye shahada kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii aliyeweza kumfichua staa, Q Jay aliyekuwa akiunda Kundi la Wakali Kwanza akiwemo sambamba na Joslin pamoja na Makamua.

 

Full Shangwe limefanikiwa kufanya naye mahojiano maalum ambapo ameongelea matukio mengi aliyopitia yenye kusikitisha na kukatisha tamaa.

 

Full Shangwe: Kuna kipindi ulikuwa na mwanamke wa Kizungu, ulikutana naye vipi?

 

D. Malick: Kuna kaka yangu mmoja anayefanya kazi nchini Malawi shirika moja la kutoa misaada, sasa siku moja walikuja nchini na Mzungu huyo anaitwa Marga Amour.
Akiwa Bongo tukawa marafiki lakini mwisho wa siku alinionesha hisia na mi nikamuonesha tukawa wapenzi.

Full Shangwe: Tetesi zilizopo ni kwamba uliachana naye, ilikuwaje?

D. Malick: (Anainama chini na kulia kwa muda). Naweza sema historia yangu ya maisha inaanzia hapo.
Baada ya kukaa na Marga (Mzungu) kwa muda mfupi aliniambia kuwa anarudi nchini mwao (Hispania) siku hiyo nikamsindikiza hadi Uwanja wa Ndege (wa Julius Nyerere), akalia sana na mimi pia.

Aliniahidi mambo mengi na kuniachia kiasi cha pesa kwa ajili ya kufanya taratibu zote ikiwezekana kwenda kusoma na kuishi naye nchini Hispania. Akaondoka zake.

 

Full Shangwe: Baada ya hapo ikawaje?

D. Malick: Siku hiyohiyo baada ya kuondoka, nikapanda daladala na kurudi zangu nyumbani. Nikiwa ndani ya daladala sijui hata ni shetani gani alinipitia, kuna dada mmoja (Zaituni) nilipanda naye siti moja, hatukuongea njia nzima lakini baada ya kushuka wote Mwenge tukajikuta tumebadilishana naye namba.

 

Mawasiliano yakaanza kunoga. Nikamueleza ukweli kuwa nina mawasiliano na Mzungu, akanishauri vingi kuwa niachane naye nikaona sawa kwa kuwa kwanza yupo mbali na mimi halafu alikuwa amenipita umri sana.

 

Full Shangwe: Na ilikuwaje sasa ukakutana na Q-Jay?

D. Malick: Q Jay nilikutana naye kipindi nipo chuo (Chuo cha Ustawi wa Jamii) na yeye alikuwa akiishi maeneo hayo ya Kijitonyama. Alikuwa katika stress zake za maisha na mimi nilikuwa naishi na Zaituni hivyo tukawa marafiki, anakuja tunashauriana nikaona sasa nifanye naye muziki rasmi nimtoe katika kuokoka.
Zaituni alikuwa mshauri wangu mkubwa na Q Jay, nikawa nauza mikaa, samaki na vingine. Kila kitu anatushauri.

 

Full Shangwe: Kuna habari kuwa wewe na Q Jay mliwahi kuiba simu Mwanza mkawekwa ndani?

 

D. Malick: Ilikuwa hivi, mimi na Q Jay tulienda Mwanza kwa ajili ya shoo ambayo tuliiandaa maeneo ya Nyegezi. Nilimuaga Zaituni wangu Dar na kuchukua nguo zangu kwa kuwa yeye ndiye alipanga nyumba na vitu vyote vilikuwa vyake.

Siku chache kabla ya shoo, tulienda sehemu kunywa, hatukuwa tunajua kitu, kuna askari mmoja alikuwa ni shabiki mkubwa.

HADITHI: SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU – SEHEMU YA 1 (Audio)

Nakuletea dakika 15 za kwanza za simulizi hii tamu ya SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install #GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee!

Android: Bofya ==>http://bit.ly/2AAQe1d
iOS: Bofya ==>http://apple.co/2Assf4M