×

Sarakasi za Uchaguzi Zaimega Chadema, Singida Wasimamisha Mgombea

SARAKASI za kisiasa zinazidi kushamiri! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia Uongozi wa Vyama Vinavyounda Umoja wa Katiba Mpya (UKAWA) kueleza kutoshiriki kwake katika uchaguzi mdogo wa ubunge Januari 13 mwakani kwa madai ya kutokuridhishwa na uchaguzi wa udiwani wa Kata 43 uliofanyika Novemba 26, uongozi wa Chadema mkoa wa Singida jana umempitisha mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho.
Tukio hilo linakuja zikiwa zimebaki siku 25 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambapo Jimbo la Singida Kaskazini, lililokuwa linakaliwa na Lazaro Nyalandu aliyekuwa CCM kabla ya kutimkia Chadema Oktoba 30. Jambo hilo limeonekana ‘kuipasua’ Chadema katika pande mbili.
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Singida, Shaban Limu amesema leo Jumanne, Desemba 19  kuwa  chama chao kimemteua Djumbe David Joseph kuwania ubunge wa Jimbo la Singida Kasakzini ambapo msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Singida naye amempitisha.
“Tutafanya kikao cha kuweka mikakati ya kampeni, tutafanya kampeni zitakazokiletea chama ushindi wa uchanguzi huo mdogo,” alisema Limu.
Wagombea wengine ni Dalphina Patrice Mlewa (CUF), Omari Mohammed Sombi (Alliance for Tanzania Farmers Party), Monko Justein Joseph (CCM), Aloyce Mohammed Nduguta (Ada Tadea) na Mchungaji Samwel Libisu (CCK) ambao walipitishwa na kutangaza jana Desemba 18, 2017 na Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Singida, Rashid Mandoa baada ya kukidhi vigezo vyote vinavyo hitajika.
Aidha Mandoa amesema wagombea kutoka vyama vya NRC na UMD wao hawakupitishwa baada ya kushindwa kukidhi vigezo. Wagombea kutoka UDP na UDPP hawakurudisha fomu.
Wakati huo, Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema; ‘’Kwa mjibu wa Katiba ya Chadema, Kamati Kuu ndiyo inayopitisha jina la mgombea na Kamati Kuu haijakutana sasa hilo jina limepatikanaje.”
“Tutashangaa hata NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) kama wataendeleza mchakato wa jina hilo na tumeagiza tuletewe taarifa na hatua zitachukuliwa kwa wahusika kwani kilichofanyika ni kosa la jinai, kama barua ya Katibu Mkuu kuthibitisha kupitishwa na Chama haipo wao wameitoa wapi,” amehoji Mrema.
Mrema ameeleza kuwa iwapo kuna watu wametumiwa basi watambue kwamba msimamo wa chama haujabadilika na wanafuatilia suala hilo na hatua zitachukuliwa kwa viongozi wote waliohusika.

HADITHI: SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU – SEHEMU YA 1 (Audio)

Nakuletea dakika 15 za kwanza za simulizi hii tamu ya SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install #GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee!

Android: Bofya ==>http://bit.ly/2AAQe1d
iOS: Bofya ==>http://apple.co/2Assf4M