×

Simulizi ya Mfungwa Aliyeishi Gerezani Miaka 55 na Kuachiwa na Magufuli Inasikitisha – Video

Mtalikidonga akifanya mahojiano na Global TV.

PEKOS Mtalikidonga (55) mfungwa aliyekuwa na umri mdogo kuhukumiwa kunyongwa akiwa na wenzake wanne akiwemo kaka yake, na baadaye kusamehewa na Rais John Magufuli Desemba 9, mwaka huu, amesema anajivunia kupata msamaha huo wa Rais wakati ambapo amefanikiwa kupata manufaa mbalimbali akiwa jela.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana, Pekos ambaye kipindi anapatwa na mkasa huo mwaka 1974 alikuwa mtoto wa miaka 12, anasema jela imeweza kumfundisha kusoma na kuandika, lakini pia imemfanya kuwa mbobezi katika ufundi wa kutengeneza sabuni.

Pekos na kaka yake wa tumbo moja, John Mtalikidonga (57), Yohana Chengula (71), Aloyce Mwalongo (80) na Raphael Mlyuka (75) walihukumiwa katika kesi ya mauaji ya mkazi wa mjini Njombe mwenye asili ya Kiasia (jina limehifadhiwa), iliyosikilizwa kuanzia mwaka 1974 na hukumu kutolewa mwaka 1978.

Aliongeza na kusema kuwa wakati anakamatwa alikuwa na umri wa miaka 14, wakati huo ilikuwa mwaka 1974 na ilipofika mwaka 1978 akahukumiwa kunyongwaakiwa na umri wa miaka 16 ingawa mahakamani walimtaja kama ana umri wa miaka 18. Jambo lililomfanya kuharibu ndoto zake na mipango yake yote ya maisha,fuatilia video hii uona kwa kina anachoeleza.

FUATILIA KISA CHOTE HAPA

HADITHI: SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU – SEHEMU YA 1 (Audio)

Nakuletea dakika 15 za kwanza za simulizi hii tamu ya SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install #GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee!

Android: Bofya ==>http://bit.ly/2AAQe1d
iOS: Bofya ==>http://apple.co/2Assf4M