Ubungo: Usafiri wa Abiria Waenda Mikoani ni Kizungumkuti
Global Publishers December 23, 2017
SHARE THIS:
Abiria wakiwa wamekaa katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo, Dar kutokana na uhaba wa mabasi katika msimu huu wa sikukuu.
KUFUATIA msimu wa sikukuu ambapo watu wengi husafiri kuelekea mikoani kwa ajiri ya kwenda kusherehekea sikukuu hizo na ndugu jamaa na marafiki, hali ya usafiri katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani, Ubungo jijini Da es Salaam imezidi kuwa ngumu kufuatia uhaba wa mabasi kituoni hapo.
Abiria wamejaa wakisubiri usafiri ambao hata hivyo hawajui endapo watapata.
Kutokana na hali hiyo, SUMATRA imeamua kutoa vibari kwa baadhi ya daladala zilizokidhi vigezo na kuziruhusu kusaidia kubeba abiria kuwapeleka mikoani. Tazama picha ushuhudie mwenyewe.
Abiria wakigombania kupanda kwenye daladala ya Mbagara Rangi 3, Simu 2000 (Mawasiliano) iliyopewa kibari cha kusafirisha abiria kwenda mikoa ya Kaskazini leo asubuhi katika Kituo cha Mabasi Ubungo. Hii ni kutokana na uhaba wa mabasi kituoni hapo.
Abiria wakiwa kwenye foleni ya kukata tiketi asubuhi hii katika Kituo cha Mabasi Ubungo, Dar kutokana na uhaba wa mabasi kituoni hapo katika msimu huu wa sikukuu.