
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Global Publishers wakiongozwa na Meneja Mkuu wao Mkuu, Abdallah Mrisho leo Desemba 30, 2017 wameungana na ndugu jamaa na marafiki kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa mdogo wa Mwandishi na Mpiga Picha Mkuu wa Kampuni hiyo, Richard Bukos, marehemu Merry Bukos.

Mwili wa marehemu Mary aliyefariki dunia Desemba 28 mwaka huu baada ya kuugua ghafla, umeagwa nyumbani kwao Mburahati jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika Makaburi ya Makulumra.

Ndugu, jamaa na marafiki wamejitokeza katika kumsindikiza katika nyumba yake ya milele ambapo mwili wa marehemu umezikwa jioni hii katika makaburi hayo.





NA DENIS MTIMA | GPL