
MSANII anayechipukia kwa kasi kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ mara baada ya kuonesha manjonjo yake Sikukuu ya Krismasi kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, mashabiki wamemshauri kukaza buti kwenye uchezaji kwani bado hajaweza kulivaa jukwaa kama wafanyavyo wasanii wengine.
Wakiongea kwa nyakat huyo walisema kuwa, kuimba hawezi kusemwa sana kwa sababu ndiyo kwanza anaingia kwenye gemu lakini akaze buti kwenye uchezaji wake ili kuwashawishi mashabiki wanaotaka kumsikiliza.
“Unajua muziki ukiingia kwa kuona aibu kwanza huwezi kuwakusanya mashabiki ni lazima kwanza uwakusanye kwa uchezaji ndio baadae wavutiwe na ngoma yako hasa kama ni mchanga kwenye gemu hili la muziki, hakuona wenzake akina Amber, Gigy Money na hata mwanamuziki Shilole? Wote hao nao walianza kwa kucheza sana,” alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Msafiri.