MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Ahmed Ollotu ‘Mzee Chilo’ ameeleza alivyochaguliwa mke ambaye hakudumu naye licha ya kubahatika kuzaa naye mtoto moja. Katika mahojiano na kipindi cha Mpaka Home kinachorushwa na chaneli namba moja ya mtandaoni ya Global TV Online, Mzee Chilo alisema kuwa, kutokana na wingi wa majukumu ikiwemo kutumia muda mwingi kusoma, alichelewa kuoa hadi alipofikisha umri wa mika 30, jambo ambalo lilianza kuwatia wasiwasi watu wake wa karibu. Alisema kuwa, jirani yake alimfuata na kumuuliza kama yuko tayari amtafutie:
“Nilidhani utani, nikamkubalia, siku moja aliniambia nimsindikize mahali, tukafika kwenye mji mmoja na kukuta binti akatuhudumia soda na baadaye yule jirani aliniambia ninamuonaje kama nitaoa, nikakubali na kuanzia hapo akawa mke wangu, lakini hatukudumu.”
Stori: Brighton Masalu, Dar