MTANDAO wa Instagram wa Global Publishers imemtangaza mshindi wa Simu mpya ya kisasa smartphone aina ya Tecnoi Camon CX anayetumia instagram akaunti ya brity59 ambaye ameshinda baada ya kuwabwaga wenzake 53.
Katika shindano hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tecno, droo hiyo iliyochezeshwa kwa wazi, droo tano ndogo zilichezeshwa ambapo washindi wa kila droo waliingizwa kwenye droo kubwa ya fainali ambayo mshindi mmoja aliyejulikana kwa jina la brity59 ndiye amejishindia simu hiyo.
Mshindi anatakiwa kuwasiliana nasi kupitia DM ya instagram yetu, WahtsApp 0753 715 779 au apige simu namba 073 479 875 ili kupewa maelekezo ya kuipata simu yake.
Vigezo na masharti ya shindano yanaendelea kuzingatiwa.