×

TPA YABAINI WIZI MKUBWA WA MAFUTA BOMBA LA ‘SPM’

Miudombinu ya wizi ilivyotengenezwa.

Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakishirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania wanamshikilia Ndg. Samwel Nzagi Kilang’ani mwenye umri wa miaka 63 kwa tuhuma ya kutoboa Bomba la mafuta ya Dizeli la “Single Point Mooring” mali ya TPA na kujiunganishia bomba lake la mafuta hadi kwenye nyumba yake ambako ameweka matanki makubwa ambayo ameyachimbia chini.

Hali yenyewe.

Kwa sasa Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa hatua za uchunguzi na sheria huku watuhumiwa wengine wakitafutwa.

 

Bomba limeunganishwa kwenye nyumba ya mtu.