
WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema), Edward Lowassa amekutana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ili kumpa mrejesho wa alichozungumza na Rais Dkt. John Magufuli juzi Januari 9, alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu nwa taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Msemaji wa Lowassa imeeleza kuwa kumekuwa na taarifa nyingi za kuupotosha umma kuhusu ziara ya Lowassa kwenda Ikulu na nyingine zikisemwa zimetoka kwa msemaji wake.
VIDEO: SHUHUDIA LOWASSA ALIVYOTINGA IKULU
“Taarifa zote hizo siyo kweli na wala siyo rasmi kutoka ofisini kwa Mh. Lowassa. Baada ya ziara ile, Mhe Lowassa alikutana na mwenyekiti wa chama chake, Mhe Freeman Mbowe na kumpa mrejesho wa yaliyojiri Ikulu.”
MRISHO GAMBO AANIKA SIRI YA LOWASSA KUONANA NA JPM
“Kumekuwa na taarifa nyingi kwenye mitandao zikiwemo kufunguliwa kwa akaunti mbalimbali feki , taarifa zote hizo zipuuzwe kwani zina lengo la kupotosha kwa malengo wanayoyajua wapotoshaji hao pamoja na mawakala wao,”
“Taarifa rasmi zitatolewa kwa njia rasmi na watu wenye mamlaka hiyo.poleni kwa usumbufu wote.”
Imeeleza taarifa hiyo.