×

Shoo ya PAPII kwa Wabunge, Mawaziri, Acha Kabisa! (Pichaz + Video)

Msanii mahiri wa muziki wa Dansi, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ akitoa burudani katika sherehe ya harusi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa (DAS), Joseph Chitinka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mbezi Garden jijini Dar.

 

ACHA KABISA! Kwa mara ya kwanza tangu atoke jela, msanii mahiri wa muziki wa Dansi, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ hivi karibuni aliacha gumzo baada ya kufanya shoo ya aina yake huku akiwadatisha mawaziri, wabunge, Risasi Mchanganyiko linakuripotia.

 

ILIKUWA HIVI

Chanzo makini kilichokuwa kwenye tukio hilo kilieleza kuwa, Papii alifanya shoo hiyo Jumamosi iliyopita katika sherehe ya harusi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa (DAS), Joseph Chitinka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mbezi Garden jijini Dar.

 

Kiliendelea kusimulia kuwa, harusi hiyo ilikuwa ni ya aina yake na ya kipekee kutokana na wingi wa vigogo wa serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) huku Papii akiongeza mvuto zaidi baada ya kuibuka ukumbini kama sapraizi.

Wabunge wakiendelea kufanya yao.

“Yaani ilikuwa ni harusi kubwa sana…walikuwepo vigogo wengi sana wa serikali wakiwemo mawaziri na wabunge ambao walidatishwa vilivyo na shoo ya nguvu aliyoifanya Papii ukumbini hapo,” kilisema chanzo hicho.

…Papii akitunzwa mihela.

VIONGOZI WA SERIKALI NDANI

Mtoa ubuyu aliwataja viongozi wa serikali waliokuwepo kwenye harusi hiyo kuwa ni Spika wa Bunge, Tulia Akson, Antony Mavunde, Angelina Mabula, Mwenyekiti wa Uvccm, Catherine Magige na viongozi wengine wengi.

Burudani ikiendelea.

“Kiukweli watu walikula na kunywa na kusaza kwani chakula kilikuwa ni kingi pamoja na vinywaji vya kila aina hivyo hakuna aliyetoka bila kula au kunywa alichokitaka,” kilieleza chanzo.

 

PAPII APAGAWISHA

Papii ambaye aliambatana na kada mmoja wa CCM alipopewa kipaza sauti ‘mic’ alianza kwa kumshukuru Rais Magufuli pamoja na Wanaccm wenzake kisha akaanza kutoa burudani yake ya kwanza tangu atoke jela ambapo burudani hiyo ilikuwa ya aina yake kwani kila mtu alinyanyuka kwenye kiti na kucheza.

 

“Ni kweli ng’ombe hazeeki maini maana shoo aliyofanya Papii kwenye hii harusi ilikuwa ni patashika yaani mawaziri, wabunge na viongozi wengine wa serikali waliokuwepo walipagawa vilivyo, niliamini kuwa kipaji hakifi hata mtu apelekwe wapi aisee,” kilisema chanzo.

Papii akiwa na washikaji zake.

AMWAGIWA MINOTI

Kutokana na shoo hiyo ya aina yake na wageni waalikwa wakiwemo viongozi hao wa serikali kufurahishwa nayo, walianza kumtuza ‘mahela mengi mpaka akashindwa kuyashika vizuri mkononi.

 

“Mahela aliyotuzwa Papii ni mengi sana kwa kweli maana alishindwa kuyashika mikononi na kuyaweka kwenye mifuko ya suruali na siyo fedha ndogondogo bali ni noti za elfu kumikumi, hii yote ilitokana na kwamba aliwafurahisha watu kwa muziki wake ambao waliumis kwa muda mrefu,” kilimalizia chanzo.

 

PAPII ANAIZUNGUMZIAJE SHOO HIYO

Ili kujua alijisikiaje kufanya shoo ya kwanza tangu atoke jela kwenye harusi iliyokuwa na vigogo wengi wa serikalini, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Papii kwa njia ya simu lakini iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Wakicheza muziki.

TUJIKUMBUSHE

Desemba 2017, Rais John Pombe Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa mbalimbali ambapo kati yao walikuwepo wanamuziki wa Dansi, Papii na baba yake Babu Seya ambao walihukumiwa kifungo cha maisha jela ambapo tangu watoke hawajafanya shoo sehemu yoyote na Papii hii ni mara yake ya kwanza kuimba kwenye harusi ya kigogo huyo.