×

Mambosasa Akanusha Kwasaka Wavaa Vimini na Wenye Viduku

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema habari iliyochapishwa na Gazeti la Nipashe kwamba leo Januari 17, 2017 yenye kichwa cha habari “Polisi wanawakamata wavaa vimini na wanyoa viduku” imepikwa na si ya kweli.
Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Dar, Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na wanahabari huku akisema mwandishi (na gazeti lake) wanatafuta umaarufu kwa kutengeneza stori na kuwataka awambie Watanzania kwamba habari hiyo haikuwa ya kweli.

 

“Sikueleza kwamba kuna msako unaoendelea wa kukamata watu wanaovaa vimini na kunyoa viduku, isipokuwa nilisema mtu anaweza kuyafanya matendo ambayo ni kinyume cha maadili ya Tanzania. Kilichoandikwa ni uzushi, mwandishi amechukua maneno akaweka kinywani kwangu ili niyaseme akauze gazeti,” alisema Mambosasa.