×

Amanda Adaiwa Kufichwa na Bwana Uingereza

STAA wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ baada ya kupotea Bongo kwa muda wa miezi miwili sasa, inadaiwa amepelekwa Uingereza na mwanaume ambaye ndiye awali alimfungulia biashara ya saluni.

 

Chanzo makini ambacho kipo karibu na staa huyo kilichoomba hifadhi ya jina kilidai kuwa, Amanda baada ya saluni yake kubuma bwana wake huyo aliamua kumchukua mazima ambapo kwa sasa wapo Uingereza wakifanya michakato ya kuchukuana jumla.

 

“Amanda kafichwa na mwanaume huko Uingereza, ndiyo maana hammuoni. Na hivi karibuni mtasikia habari njema kwani wanafanya mipango ya kuoana,” kilidai chanzo.

Amanda alipotafutwa na kupatikana alisema: “Kwanza habari hizo sijazipenda kabisa, huku nimekuja kwa starehe zangu na sitokaa nikaweka wazi mambo yangu, hiyo haihusiani kabisa,” alisema Amanda.

STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi.