×

IGP Sirro Asema Vijana 60 wa Tanzania Wamekamatwa Msumbiji

Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) Simon Sirro amekuatana na viongozi wa dini leo na kuzungumza na vyombo vya habari ambapo amesema Ushirikiano waliokubaliana kufanya kati ya Jeshi la Polisi la Tanzania na la Msumbiji Polisi kukabiliana na uhalifu unaojitokeza kati ya nchi hizi jirani umezaa matunda

IGP Sirro amesema awali alitangaza kuna watu waliokuwa wanajihusisha na mauaji ya Kibiti wamekimbilia Msumbiji na ametaarifu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Msumbiji amemweleza Polisi wa nchi hiyo wamefanikiwa kukamata vijana takribani 60 msituni wengi wao wakiwa Watanzania wakihusishwa na vitendo vya kihalifu

Sirro ameeleza jambo jingine kuwa ameona ana miezi saba toka awe IGP na kuona awaite waandishi ili wajue jeshi hilo linaenda salama.

FUATILIA IGP SIRRO AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA DINI