KUTOKA IKULU: Rais John Magufuli amepokea kwa huzuni na masikitiko taarifa za kifo cha mmoja wa waasisi wa Taifa, Kingunge Ngombale Mwiru kilichotokea usiku wa kuamkia leo. Rais amesema Taifa limepoteza mtu muhimu na mwenye mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa la Tanzania.
“Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ametoa mchango mkubwa, sisi kama Taifa hatuwezi kusahau na tutayaenzi mema yote aliyoyafanya wakati wa utumishi wake uliotukuka,” amesema Rais Magufuli.
