Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amewapatia viwanja mabalozi 65 ambao wapo tayari kuhamia Dodoma ambapo watalazimika kuvijenga kwa fedha zao wenyewe.
Pia Rais magufuli amewataka mabalozi hao kutembelea vivutio mbalimbali vinavyopatatikana nchini huku akiwahimiza kuwakaribisha watalii wa nchi zao kutembelea tanzania.
Rais Magufuli amewaambia mabalozi hao kuwa serikali yake inawapenda wawekezaji kutoka nchi mbalimbali na kuwakaribisha waje kuwekeza hapa nchini. Rais Magufuli ameyasema hayo katika hafla ya Mabalozi(SHERRY PARTY) Ambapo mwakani sherehe kama hiyo itafanyika mjini Dodoma.