×

Taharuki: Lori Lenye Shehena ya Sementi Nusura Liue

LORI la mizigo  lililokuwa limebeba sehena ya saruji limezua taharuki kwa wakazi wa Jiji la Mbeya baada ya kushindwa kupandisha mlima wakati wakati likisafirisha mzigo huo.

Tukio hilo limetokea leo Jumatatu, Feb 26, 2018 majira ya saa mbili asubuhi katika Barabara  Mbeya – Tunduma iliyopo Milima ya Iwambi mkoani humo baada ya lori hilo kushindwa kupandisha mlima na kuanza kurudi nyuma, hali ambayo ilisababisha wapitanjia na wenye magari kulikwepa haraka vinginevyo lingesababisha ajali kubwa na pengine kuua kabisa.

Baadaye gari hilo lilikwama na kuziba njia, hali ambayo ilisababisha adha kwa magari mengine kushindwa kupita.

Hata hivyo, baadaye lilifika lori jingine eneo hilo ambapo mzigo ulifaulishwa lakini abiria waliokuwa kwenye mabasi walilazimika kushuka na kutembea kwa miguu na wengine waliokuwa kwenye usafiri wao binafsi walilazimika kusubiri hadi lori hilo litolewe.

PICHA: Global TV Ripota, Mbeya