
ZIKIWA zimetimia ni siku 100 tangu kupotea kwa mwandishi wa Mwananchi Communication Ltd, Azory Gwanda, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana wilayani Kibiti, mkoani Pwani, uongozi wa kampuni hiyo wametoa mrejesho kuhusu hatua iliyofikiwa ya kumtafuta mwandishi huyo.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni, Mkurugenzi wa Mwananchi, Francis Nanai amesema kuwa mpaka sasa hawajajua mwandishi huyo yuko wapi, na hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa vyombo vya usalama.

Pia, Mwananchi wametoa rai wakiomba wandishi huyo arejeshwe akiwa mzima, huku kampuni hiyo ikijitolea kwa ajili ya familia ya Azory, kuwalipia watoto ada, kumfungulia biashara mkewe itakayomuwezesha kuendesha maisha katika kipindi hiki kigumu hasa ikizingatiwa ametoka kujifungua.
Aidha, wametoa rai kwa Watanzania kumchangia mama huyo ili kulisukuma gurudumu la maisha katika kipindi hiki cha upweke mpaka pale mumewe atakapopatikana.