


MIUNDOMBINU ya barabara iliyokuwa korofi katika eneo la kuingia stendi ya Makumbusho jijini Dar na mitaa mingine inayozunguka stendi hiyo imekuwa kivutio kwa watumiaji baada ya kukarabatiwa.
Mtandao wa Global Publishers umepita eneo hilo na kushuhudia miundombinu hiyo ikiwa tayari imejengwa tofauti na hapo awali ilivyokuwa ikisumbua kwa waendeshaji wa daladala za kuingia pamoja na watembea kwa miguu hususan nyakati za kipindi cha mvua kwani hakukuwa na lami.
NA DENIS MTIMA/GPL