MWANAMUZIKI mahiri wa dansi Bongo, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ ambaye sauti yake ilimisika kwa muda kwa miaka 14, amefunguka kuwa, hataki kabisa kuzungumzia yaliopita kwani si ndwele, badala yake anaangalia mambo ya mbeleni zaidi.
Papii aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kwa sasa anaamua kupiga kazi tu kwani tayari ameshatengeneza nyimbo tatu ambazo tayari ameachia moja inayokwenda kwa jina la Waambie.
“Sitaki kufikiria kabisa yaliopita. Baba Magufuli (rais) ameshasema hapa kazi tu na ndivyo nitakavyofanya,” alisema Papii.
Papii aliongeza kuwa, mashabiki wake wajitokeze Machi 10, mwaka huu kwenye Ukumbi wa King Solomon, Namanga, Dar wapate ladha halisi waliyoikosa kwa muda mrefu.