×

Enock Bella Alamba Shavu Burundi – Video

 

MSANII wa Bongo Fleva, Enock Bella anayetamba kwa nyimbo mbalimabli kama Sauda, Ngoja Kidogo na zingine nyingi hivi amelamba mkataba wa nguvu kutoka kampuni ya CHAKOR Music Group ya nchini Burundi itakayokuwa ikisimamia kazi zake za muziki.

 

Akizungumza wakati wa kumsainisha Enock, Meneja wa Chakor Music, Kenth alisema kampuni yao ina wasanii wengi wa Afrika Mashariki, lakini wameingia Tanzania kujitanua na ku-push muziki wa bongo Fleva.

 

“Tumeingia Tanzania kusaka wasanii wenye vipaji tunaoweza kuwasimamia, tukanona Enock ana uwezo mkubwa, kazi zake tumezifuatilia ana sauti nzuri, anajua kuimba na anajua muziki, hivyo tunaamini tutafika naye mbali. Tunapenda kufanya kazi na Enock Bella kwa sababu ana radha tofauti katika uimbaji na kutunga mashairi,” alisema Kenth.

 

Kwa upande wa Enock ambaye amesaini mkataba huo wa miaka mitatu ameshukuru kupata management mpya ya kumuongoza kimuziki baada ya kundi lao la YAMOTO Band kuvunjika;

“Sikujua kama kazi ninayoifanya inapenya hadi mbali. Namshukuru Mungu nimepata management, nawashukuru pia Chakor Music kwa kuona kipaji na mchango wangu kwenye tasnia ya muziki. Naamini sasa nitafanya muziki ufike mbali zaidi ya vile nilivyokuwa nikifanya mwanzo, mkataba ni mzuri, tukishirikiana kwa pamoja tutafika pale tunapopataka,” alisema Enock Bella.

 

VIDEO YA TUKIO HILO