×

Mfaransa Simba Awapumzisha Wachezaji, Waanza Maandalizi

KOCHA Mfaransa wa Simba, Pierre Lechantre amewapumzi­sha wachezaji wake kwa takrib­ani saa tano ili kuhakikisha wanakuwa vizuri kabla ya kuanza maan­dalizi ya mwisho.

Simba iko mjini hapa tayari kuivaa Al Masry katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya sare ya 2-2 jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kusafiri kwa zaidi ya saa nane kutoka Dar es Salaam kupitia Addis Ababa, Ethio­pia halafu Cairo, Misri na baadaye hapa, Lechan­tre aliamua kuwapumzisha wachezaji hao.

Kwanza wali­fikia kupata ki­fungua kinywa na baada ya hapo wakaanza mapumz i k o kabla ya kuanza maandalizi ras­mi jana usiku.

Wacheza j i hao wameanza maandalizi ya mwisho jana usiku baada ya Mfaransa huyo kutaka wajifue usiku.

Wakati mechi inatarajia kuan­za saa moja usi­ku, yeye alitaka wachezaji wake kuanza mazoezi mapema zaidi.

Simba im­eanza kufanya mazoezi jioni ili kuhakikisha ina­zoea mazingira na hali ya hewa kabla ya ku­wavaa Al Masry.