JUHUDI za kuwaunganisha Watanzania na ulimwengu unaotuzunguka ni muhimu, kwani kuna watu milioni 14 nchini wanaoishi katika maeneo ambayo hayajaunganishwa na mtandao wa Internet.
#CaseForChange imetembea na Neema kutoka thebongolese.com hadi kijiji cha Nyombo village – moja ya vijiji vilivyo sehemu za ndani kabisa nchini, na kikiwa kimoja miongoni mwa vijiji vilivyounganishwa na mtandao huo, ambako imekutana na wakazi wake watatu ambao maisha yao yamebadilika na kuwa mema kutokana na kuunganishwa huko.
Hadji anaweza kupata habari za masomo kupitia mfumo wa Tehama unaoweza kuwa kwenye simu au kompyuta. Godfrey hivi sasa anaweza kupakua muziki mpya mara tu unapotoka na anaweza kujiunga na mazungumzo yanayofanyika katika mitandao ya kijamii. Anthony anashughulikia mavuno na kupanga bei nzuri kutokana na uwekezaji huo.
Mahojiano ya Neema yanajikita katika utafiti wa simulizi za watu watatu miongoni mwa simulizi binafsi zinazofichua njia ambazo zimeleta mabadiliko yanayotokana na kuunganishwa na Internet kwa upande wa wakazi hao katika kujifunza mambo mbalimbali na kuendesha biashara.
Kama anavyosema Hadji, fursa ya kutafuta habari mbalimbali inaifanya dunia ambayo ni kubwa, kuwa “kama kijiji tu”.
Hivyo, tazama unavyoweza kushiriki kwa upande wako na kusaidia kubadili maisha ya mamilioni ya watu.
Hatua hii muhimu ya mwanzo ya ushirikiano baina ya Airtel, Tigo na Vodacom imewapatia fursa watu 73,000 wanaoishi vijijini kama kile cha Nyombo kujiunga na Internet.
Huo ni mwanzo tu wa safari yetu ambayo ndiyo kwanza imeanza. Kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko makubwa.
Tusaidie katika kupitia #CaseForChange.
+ Instagram: https://instagram.com/caseforchange
+ Facebook: https://facebook.com/caseforchange
+ Twitter: https://twitter.com/caseforchange
+ Website: http://caseforchange.com