MWANAMAMA mkali kwenye Bongo Movies, Kajala Masanja ‘Kay’ amesema kuwa, ukimya wake unatokana na umri wake alionao kwa sasa (miaka 35) ambao anaona wazi umesogea hivyo ni vyema kujituliza na siyo kurandaranda kama zamani.
Kajala aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, anaona umri wake umekwenda, lakini pamoja na hayo ni kwamba, mtoto wake, Paula ambaye yuko kidato cha nne sasa, ameshakua mkubwa hivyo ni vyema kutulia.
“Mambo ya kwenda kwenye majumba ya starehe yamepitwa na wakati kwa sababu Paula ameshakuwa msichana mkubwa, ni bora kutulia sasa,” alisema Kajala.
IMELDA MTEMA, DAR