×

CELINE DION Kufanyiwa Upasuaji wa Sikio!

MWANAMAMA ambaye ni mkongwe katika Muziki wa Pop,Celine Dion amelazimika kupiga chini kwa maranyingine shoo aliyotarajia kufanya katika Ukumbi wa Colosseum huko Caesars, Las Vegas, tarehe 27 ya mwezi huu na shoo nyingine ya tarehe 17, mwezi ujao, kutokana na kuugua sikio na anatarajia kufanyiwa upasuaji.

 

Tatizo hilo la kusumbuliwa na sikio la upande wa kushoto,limemsababishia Celine kupiga chini shoo mbilimwezi Januari na kutokana na ukubwa wa tatizo atalazimika kufanyiwa upasuaji.

 

“Ninasumbuliwa sana na sikio langu kiasi kwamba siwezi kusikia vizuri wakati wa kufanya shoo,nilitamani mno kuwana watu wa Las Vegas, wiki ijayo lakini nashindwa. Mungu ni mwema nitakuwa nao siku zijazo,” alisema Celine Dion alipokuwa akihojiwa na Mtandao wa Billboard.

Las Vegas, Marekani.