Mchekeshaji aliyejizolea umaarufu mkubwa Bongo kutokana na Clip zake za vichekesho kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Dullvan, amehudhuria moja ya shoo zilizoandaliwa na ukumbi wa Taifa wa Burudani, Dar Live, uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.
Dullvan aliamsha popo mara tu alipopanda stejini na kucheka kicheko chake ambacho hukitumia mara zote kwenye vichekesho vyake, hali iliyowafanya mashabiki kushangilia na baadaye akaamsha popo tena kwa kucheza na kuwaimbisha mashabiki ngoma za singeli.