
Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM iliyokutana kwa dharura leo mchana chini ya Mwenyekiti UVCCM, Kheri James imetengua uteuzi wa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi-UVCCM Taifa, Jokate Mwegelo kuanzia leo Machi 25, 2018

Jokate atabaki kuwa mwanachama wa kawaida na nafasi yake itajazwa baadae. Hakuna sababu iliyotolewa juu ya kutengua uteuzi huo.