Ofisa Habari wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tumaini Makene, amesema Kamati Kuu ya Chama hicho imekutana kwa dhalula kujadili kuhusiana na kesi inayowakabili baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe, ambao mpaka sasa wapo rumande, kwa tuhuma za uchochezi, uasi na kuhamasisha chuki.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 28, Makene amesema jambo la kuwaweka ndani viongozi wakuu wa chama cha upinzani, siyo jambo dogo na pia sababu za kuwafutia dhamana hazikuwa sababu za msingi hivyo kamati kuu ya chama hicho imeamua kujadili kwa kina na kisha watatoa maamuzi yao juu ya suala hilo.