×

UEFA YABADILI KANUNI YA ‘SUB’ KUWA WACHEZAJI WANNE

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya (UEFA) linatarajiwa kufanya mabadiliko kadhaa katika uendeshaji wa mechi za michuano yake ikiwemo kuruhusu mabadiliko ya mchezaji wa nne katika mechi moja.

Sehemu ya mabadiliko hayo pia itahusisha mchezaji kuruhusiwa kuzichezea timu mbili katika michuano ya msimu mmoja ikitokea akahama.

 

Imeelezwa kuwa mchezaji wa nne ataruhusiwa kuingia katika muda wa dakika za nyongeza kuanzia katika hatua ya mtoano. Utaratibu huo unatarajiwa kuanza kutumika msimu ujao. Kwa kanuni za sasa zilivyo, Arsenal imeshindwa kumtumia mshambuliaji PierreEmerick Aubameyang katika Europa League kwa kuwa tayari alishaichezea Borussia Dortmund.