×

LULU DIVA ETI HAJUI MUZIKI? MSIKIE!

MWANADADA anayetamba kwa sasa na ngoma ya Homa, Lulu Diva, amefunguka kwamba ingawa kuna baadhi ya watu wanadai kwamba hajui muziki lakini kwa nyimbo anazofanya anawakimbiza wanamuziki wengi sokoni na anapata shoo kibao.

 

Akipiga stori na Mikito Nusu Nusu, Lulu alisema kwamba ni kweli inawezekana hajui muziki lakini siku hadi siku anajifunza vitu vipya zaidi ambavyo vitamfanya siku moja awe bora zaidi na kufika mbali.

 

“Kuna watu huwa nawasikia wanadai kwamba sijui muziki, siwezi kubishana nao maana hilo ni suala la mtazamo tu, lakini ukweli ni kwamba ninajifunza vitu vipya siku hadi siku na nitazidi kujifunza na kuwakalisha wanamuziki wao wanaodai wanajua zaidi yangu,” alisema Lulu.

 

Stori: Boniphace Ngumije.