×

Waliokamatwa kwa Kuhamasisha Maandamano Wafikishwa Kortini – Video

Watuhumiwa wa kuhamasisha maandamano.

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema watuhumiwa waliokamatwa kwa kuhamasisha maandamano mitandaoni amefikishwa mahakamani leo Alhamisi, Aprili 5, 2018 baada ya uchunguzi kukamilika.

 

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto wakati akizungumza na wanahabari mjini humo na kusema, Mbata na wenzake ambao walitiwa mbaroni Machi 21, kwa kuhamasisha maandamano kupitia kwenye mitandao ya kijamii wakitumia simu zao za mikononi, wamefikishwa mahakamani leo na kuwataka wanahabari kufika mahakamani ili kusikiliza mashtaka watakayosomewa.

Ntuhumiwa wa bangi.

 

Aidha, jeshi hilo limewakamta watu watatu kwa kukutwa na mihuri bandia ya serikali, taasisi za fedha yakiwemo mabenki, huku wakielezwa kuwa wamekuwa wakitumia nyenzo vifaa hivyo kwa ajili ya kutekeleza matukio mbalimbali ya utapeli kwa wananchi mkoani humo.

 

Pia jeshi hilo limewakamata watuhumiwa wa madawa ya kulevya zikiwemo bangi na wengine ambao wanatuhumiwa kwa kubomoa maduka na kuiba vitu mbalimbali mkoani humo.

VIDEO: MSIKIE MUROTO AKIZUNGUMZA