
MSIMAMIZI wa kazi za staa mkubwa wa Filamu Bongo, Wema Sepetu, Neema Ndepanya amesema kuwa yeye hana desturi za kugombana na mtu na wala siyo mchokozi lakini mtu akimuanzishia analiamsha dude wakati wowote.
Akizungumza na Amani alisema kuwa baada ya Wema kushinda tuzo kulizuka maneno ambayo kamwe yeye kama mwandishi wa filamu hiyo asingeweza kunyamaza hata mara moja ndiyo maana alipambana kwa kila ambaye alikuwa akimletea dharau.
“Kikubwa mimi sipendi dharau lakini niliamua kuingia kwenye mapambano baada ya kuona kama Wema, anaonewa bila sababu nililiamsha ili tuweze kuheshimiana,” alisema Neema.
Stori: Imelda Mtema.