×

TECNO IKISHIRIKIANA NA TIGO IMEWALETEA TECNO CAMON X RASMI TANZANIA

KAMPUNI ya simu ya TECNO ikishirikiana tigo imewaletea TECNO CAMON X ikiwa ni muendelezo wa toleo la ‘CAMON’ iliyoboreshwa zaidi katika upande wa kamera ikiwa na megapixel 20 na mfumo mpya wa kunlock simu ‘FACE ID’.itakayopatikana katika maduka yote ya tigo ikiwa imeambatanishwa na kifurushi cha GB 3  kutoka mtandao wa tigo.

Kampuni ya simu ya TECNO na tigo kwa pamoja wanahakikisha mtumiaji wa TECNO CAMON X anafurahia kasi ya mtandao wa tigo. TECNO CAMON X ilitambulishwa mwezi huu  nchini Nigeria, ikiwa imeboreshwa zaidi kwenye kamera ya mbele.

 

TECNO imekua ikishirikiana zaidi na kampuni za mawasiliano kila inapokuja na toleo jipya la simu na sasa kuendeleza utamaduni huo kupitia TECNO CAMON X, ambayo ni kubwa zaidi kulinganisha na toleo lolote la ‘CAMON’. Tigo Tanzania wanaitumia nafasi hii ili kuhakikisha wateja wa kampuni zote mbili kunufaika na kasi ya 4G kutoka tigo na simu yenye ubora zaidi.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi Meneja Mahusiano wa  Kampuni ya TECNO, Eric Mkomoye, alisema “tunayo furaha kuwaletea sokoni simu yenye kamera kali zaidi ikiwa miongoni mwa toleo linalosifika zaidi upande wa kamera ambayo ni TECNO CAMON X  yenye megapixel 20 mbele na sifa nying zaidi zitakazompendeza mtumiaji wa ulimwengu wa kisasa”.

 

Mkomoye aliongeza ‘tunajivunia kushirikiana na tigo, kwani ni kampuni yenye kasi nzuri ya mtandao wa 4G na yenye ofa nzuri kwa wateja wake. Hii ni hatua nzuri katika ukuaji wa soko la simu kupitia TECNO CAMON X yenye kasi ya 4G unauhakika wa kufurahia simu yako mahali popote duniani”.

 

Naye Mkuu wa Kitengo Cha Mauzo wa Kampuni ya tigo, David Umoh, pia alipata nafasi yakuongelea ushikirikiano wao na kampuni ya simu ya TECNO.

 

 

“Dhumuni letu ni kuhakikisha soko la simu linakua zaidi Tanzania huku tukihakikisha wateja wetu wanafurahia utandawazi kupitia mtandao wetu wa 4G. na ndiyo maana tigo inakupatia ofa ya GB 3 ndani ya miezi sita kwa mtumiaji wa TECNO CAMON X”.

 

 

TECNO CAMON X inaukubwa wa kioo cha nchi 6.0, ram ya GB 3, na GB 16 memori ya ndani ya simu, megapixel 20 kamera ya mbele, megapixel 16 kamera ya nyuma na aina mpya ya ‘security’ FACE ID pamoja na alama za vidole ‘fingerprint’.