×

NAIBU SPIKA AWAONYA WANAFUNZI UDSM KUHUSU MAPENZI

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akiwahutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) kwenye Ukumbi wa Nkrumah Jijini Dar es Salaam.
Taswira ilivyoonekana ukumbini hapo wakati wakimsikiliza Dkt. Tulia.
Kongamano hilo likiendelea na wanachuo hao.
Wakimsikiliza kwa makini.

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, amewahimiza wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusoma kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao ya kielimu na kuweka pembeni masuala ya mahusiano ya kimapenzi wangali shuleni.

 

Akiwahutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) walioungana na Tawi la (DUSE) kwenye  Kongamano lililojulikana kwa jina la  ‘UNI LIFE CAMPUS PROGRAM 2018’ ambalo limefanyika katika Ukumbi wa Nkrumah Jijini Dar es Salaam, Dkt Tulia amewataka wanachuo hao kuweka masuala ya mapenzi pembeni ili waweze kutimiza ndoto zao za kielimu na kujisomea kwa bidii.

 

Na Denis Mtima/GPL.