×

LIJUAKALI: Aliyemtishia Nape Bastola si Yupo? – Video

Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali, akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani, amesema kuna mambo yanayofanyika nchini yanaleta fedheha kwa Jeshi la Polisi.

“Kuna bwana mmoja alimtishia Nape Nnauye bastola, Waziri akasema atafutwe na atashughulikiwa, huyu mtu si yupo? Na hivi karibuni ameonekana akifanya kazi tena mbele ya kamera. Hajakamatwa wala kushughulikiwa,” alisema Lijualikali na kuongeza kwamba jambo hilo linalitia doa jeshi hilo.

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA