Serikali imesema suala la Meli Mbili za Mafuta (Crude Oil) zilizokwama Bandarini kutokana na tozo ya ushuru, litapatiwa ufumbuzi ifikapo kesho, Mei 7, 2018.
Hayo yamesemwa Bungeni na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, ambaye pia amefafanua kuhusu na kupanda kwa bei ya Tende, ikiwa ni siku chache zimebaki ili waumini wa dini ya Kiislamu waanze mfungo wa mwenzi Mtukufu wa Ramadhani ambapo ndio hasa Tende huhitajika kwa wingi.