
Zifuatazo hapo chini ni sifa na kauli za Basekahino Thadeo:
JINA: BASEKAHINO THADEO
DEGREE PROGRAMME: BSc in Chemistry, 2nd Year.
NAFASI ANAYOGOMBEA: Mwenyekiti wa Kitivo cha Sayansi Asilia na Matumizi (CoNAS) Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam 2018/19.
VIPAUMBELE (SERA) NITAKAVYOTEKELEZA:
- Kuanzisha na kuendeleza CoNAS – members Associations kwa kuhamasisha kila kozi (faculty) kuwa na association iliyosajiliwa na office ya Dean of Students ili kuwa na platform ya kuweza kupaza sauti zao pia kuanzisha vikundi vya kitaaluma na kimichezo vinavyotambulika kisheria ili kuwa na nguvu moja kama wana DARUSO – CoNAS.
- Kutatua tatizo la field kwa kozi ambazo si za ualimu ili department husika ziwasaidie wanafunzi kutafuta maeneo ya kufanyia field na sio kuacha jukumu hilo mikononi kwa wanafunzi.
- Kutilia mkazo suala la usalama wa wanafunzi wanapokuwa maabara hasa upatikanaji wa vifaa vya kujikinga kama gloves, protective eye lids, mouth masks n.k
- Kuanzisha blogu/website ya wanafunzi wa DARUSO – CoNAS ambayo itasaidia upatikanaji wa taarifa muhimu kama coursework results kwa wakati husika pamoja na kuwaunganisha wana CoNAS kuwa kitu kimoja.
- Nitahakikisha naandaa makongamano maalumu kwa kuwakutanisha wana DARUSO – CoNAS na taasisi binafsi pamoja na taasisi za umma zinazojikita na masuala ya elimu nchini kama TWAWEZA ili kuweza kuongea na wanachuo juu ya changamoto za ajira na elimu zilizopo mitaani ili kuwajenga zaidi wanachuo kitaaluma na kisaikolojia kwa kujiandaa kukabili changamoto zilizopo mtaani.
- Nitahakikisha naanzisha programme maalum ya kuwakutanisha wana-CoNAS na wajasiriamali wakubwa kabisa nchini kama akina Eric Shigongo na wengineo wengi ili ku-share elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa chuo hasahasa finalists.
- Kwa kushirikiana na katibu wangu Mheshimiwa Lucas Asifiwe Moses ambaye naamini mtamchagua kwa kishindo kikubwa na naomba sana mmchague awe katibu wangu na nitahakikisha mambo ya msingi kama tatizo la ufinyu wa muda wa kujisajili ARIS, ucheleweshaji wa ID, ucheleweshaji wa bima, ucheleweshaji wa coursework, ubovu wa baadhi ya miundombinu pamoja na muingilianao wa vipindi yanatatuliwa kwa uharaka zaidi kadiri ya uwezo wetu na ushirikiano wenu wana DARUSO – CoNAS kwa makini kabisa.
Ewe mwana DARUSO – CoNAS hakikisha unafanya maamuzi sahihi kwa kunipigia kura mimi Basekahino Thadeo niwe mwenyekiti wa CoNAS kwa maendeleo ya Kitivo cha Sayansi Asilia na Matumizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“None of us is smart as all of us” VOTE FOR BASEKAHINO THADEO.