×

KHADIJA KOPA, BARNABA WANOGESHA FAINALI YA ‘TOKA NA MAIKI’ (PICHA +VIDEO)

 

Mmoja wa washiriki wa shindano la Toka na Maiki, akisoma taarifa ya habari mbele ya majaji ambao hawapo pichani.
Country Boy akikamua.
Enock Bella akiimba kwa hisia.
Barnabas akiwaimbisha mashabiki.
Enock Bella akiendelea kukamua.
Khadija Kopa naye akiwachagiza mashabiki wa burudani.
Mtangazaji nyota Dida akitafakuri jambo kwa hisia kali.
Chemical naye akifanya yake.

WAKALI  wa burudani, Malkia wa Mipasho Khadija Kopa, Barnabas Elius, Country Boy na wengine walinogesha kwa kiwango cha juu zaidi fainali ya kutafuta vijana wenye vipaji vya kutangaza kutoka mitaani iliyokuwa ikiendeshwa na Radio Times FM ikienda kwa jina la Toka na Maiki.

Mchuano huo uliwashindanisha vijana zaidi ya 300 wenye vipaji vya utangazaji kutoka mikoa mbalimbali na kuwachuja mpaka kufikia 30 ambao waliingia kwenye fainali hiyo iliyowaibua watangazaji watatu kati yao ambao wamelamba ajira ya kudumu kwenye kituo cha redio cha Radio Times FM.

Fainali hiyo iliyokuwa ya kukata na shoka ilifanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

 

Wakati washiriki hao wakionyesha vipaji vyao, wakati wa mapumziko wakali wa burudani nao walikuwa wakitumia nafasi hiyo kutoa burudani  ambapo aliyeanza kuvamia jukwaa alikuwa ni Country Boy akifuatiwa na Chemical, akaja Khadija Kopa, akifuatiwa na Barnabas na wengineo wengi.

 

Katika kinyang’anyiro hicho walioibuka washindi na kuingia mkataba wa kudumu wa kuitumikia radio hiyo ni: Ramadhani Tembo wa Dar, Amina Bilia wa Mbeya na Geofrey Pangapanga ambao walitangazwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa (Basata) Geofrey Mungereza, aliyekuwa mgeni rasmi.

Baada ya watangazaji hao wapya kujitwalia ajira hizo Khadija Kopa, Barnabas na wasanii wengine waliendeleza burudani mpaka majogoo.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL