
BAADA ya kusumbua na Wimbo wa Mbegu za Amani akiwa amemshirikisha msanii wa Bongo Fleva, Ruta Bushoke, msanii wa Nyimbo za Injili na Kuhamasisha Amani, Luundo Dunia ameachia wimbo mpya uitwao Baba Pokea Sifa wenye lugha nne.


Akizungumza na Global Tv Online, Luundo ambaye makazi yake ni nchini Canada alisema wimbo huo umetumia lugha za Kifaransa, Kilingala, Kingereza pamoja na Kiswahili.
“Malengo yangu kwa jamii ni kufikisha ujumbe wa kuhamasisha amani. Nipo katika mpango wa kuja na albamu ambayo Mungu akipenda nitawashirikisha wasanii wengi nchini akiwemo Christina Shusho. Wimbo wa Pokea Sifa video yake imefanywa na Debro,” alisema Luundo.