×

Kauli ya Sugu Kuhusu Kukiukwa kwa Misingi ya Mwalimu Nyerere – Video

MBUNGE wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema kwa zama hizi sera ya Ushirikiano wa Kimataifa nchini imebadilika ikilinganishwa na Sera hiyo kwa kipindi cha uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

 

Sugu ameyasema hayo Bungeni wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa chini ya Waziri, Balozi Augustino Mahiga.

 

Sugu amesema enzi za Mwalimu alifunga ubalozi wa Israel akiunga mkono jitihada za kujikomboa kwa Palestina, lakini sasa hivi Serikali imedhamiria kuufungua ubalozi huo, pia amedai Mwalimu alivunja Mahusiano na Morocco lakini Serikali imeyafufua hivyo akasema misingi ya muasisi wa Taifa kwa Sera za kigeni imeanza kufifia.

 

Aidha, Mbunge huyo ameitaka Serikali kuruhusu Uraia Pacha (Diaspora) ili kuwapa nafasi Watanzania waishio nje kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na si kuwakaribisha kwenye makongamano ya Zanzibar pekee.

 

Hata hivyo Sugu alitaja faida moja tu kati ya nyingi zitakazopatikana baada ya kufufuliwa kwa balozi hizo ikiwemo nchi ya Morocco kujenga Uwanja wa Kisasa wa Mpira jijini Dodoma, viwanja vya ndege, viwanda vya madawa, kukuza ushirikiano, mshikamano na kukuza uchumi kati ya nchi hizo, majeshi kubadilishana uzoefu na mengine mengi.

VIDEO: MSIKIE SUGU AKIZUNGUMZA