×

UN, VIJANA WAJADILI KUHUSU FURSA

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la  Umoja wa Mataifa- UN, Alvaro Rodriguez akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea kwenye kongamano hilo.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la  Umoja wa Mataifa- UN, Alvaro Rodriguez akiendelea na ufafanuzi.
Hafla hiyo ikiendelea.

VIJANA Mbalimbali hapa nchini leo wamekusanyika katika kongamano la kujadili  malengo 17 ya Dunia, yanayozungumzia fursa za maendeleo ya milenia, utekelezaji wake na changamoto zake.

 

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Makumbusho ya Taifa Posta jijini Dar es Salaam, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la  Umoja wa Mataifa- UN, Alvaro Rodriguez alisema kuwa malengo ya dunia ni ajenda muhimu sana kwa Tanzania, Afrika na Ulimwengu mzima.

 

Bwana Rodriguez alisema ajenda hiyo imelenga kuleta mabadiliko chanya kwa kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika utekelezaji wake wa malengo 17 ya millenia hasa ifikapo 2030.

 

Katika hafla hiyo vijana wamefundishwa malengo makuu matatu ya ambayo ni namana ya kuwawezesha vijana kuwa na uwezo wa kuendesha shughuli zao na kutumia fursa zinazowazunguka.

 

Pia vijana hao  wametakiwa  kuwa wabunifu katika kutimiza malengo hayo 17 ya dunia ikiwa ni pamoja na kuwa wabunifu na kufuatilia yale waliyoyapanga na kuyatekeleza.