×

Sister Fay Awaangukia Watanzania

Faidha Omary ‘Sister Fay’

WAKATI waumini wa Dini ya Kiislam wakiendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, msanii wa muziki na filamu Bongo, Faidha Omary ‘Sister Fay’ amewaangukia Watanzania kutokana na kukaa nusu utupu.

 

Akipiga stori na Za Motomoto News, Sister Fay alisema, kwa kuwa mwezi huu ni wa toba, anawaomba radhi Watanzania wote aliowakwaza kwa kukaa nusu utupu mitandaoni kwani ile ilikuwa ni katika kutafuta kiki ili kupata umaarufu na kuweza kuendesha maisha.

 

“Huu ni mwezi wa toba, ninawaomba Watanzania na mashabiki wangu kwa jumla wanisamehe kwa kukaa kwangu nusu utupu mitandaoni ile ilikuwa ninatafuta kiki tu, lakini imenitokea puani kwani nimejikuta nikiwakwaza watu wengi sana, sitarudia tena nimejifunza,” alisema Sister Fay. ni kuambulia maumivu tu, hakuna cha maana zaidi.

 

“Ningekuwa nimepata nafasi ya kumshauri Mobeto, ningemwambia asimrudie Diamond, lakini ndiyo hivyo nilisikia wako pamoja tena, ninachoweza kumwambia ni awe makini tu maana penzi na staa linaumiza sana. Kwani ni watu ambao hawatulii, atajikuta anajipotezea muda na baadaye kuja kujuta.

“Nimewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa, uliniumiza sana na ndiyo maana nampa somo Mobeto kuwa makini sana ili kukwepa kuumiza moyo wake na kupoteza muda,” alisema Johari.

Stori: Gladness Mallya.