×

MAKONDA APOKEA TENDE, AAHIDI KUWAPELEKEA YATIMA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  akipokea tende kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Miraji Islamic Centre, Arif Yusuph.
Wakiziangalia tende.

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  leo amepokea shehena ya Tende kutoka Taasisi ya Darul Irshaid Islamic kwa kushirikiana na Miraji Islamic Centre kama sehemu ya sadaka kwa Waislamu katika kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

 

Makonda amesema tende hizo zitatolewa kwa vituo vya watoto yatima na waishio katika mazingira magumu vilivyopo jijini Dar es salaam.

 

Aidha amewasihi kinadada kuheshimu imani za watu kwa kujisitiri na kuvaa nguo za heshima ili kuepuka kuharibia watu Swaumu.

 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Miraji Islamic Centre, Arif Yusuph,   amesema wameamua kutoa tende hizo ikiwa sadaka kwa Mwezi wa Ramadhan.