
Michuano ya timu za mitaani maarufu kama Ndondo CUP jana ilizinduliwa rasmi kwenye Uwanja wa Kinesi uliopo Ubungo Shekilango Jijini Dar ambapo sasa pamoja na wadhamini wengine utadhaminiwa pia na Benki ya DCB kupitia huduma yao mpya ya Digital Account.

Akizungumza balozi wa DCB Benki ambaye ni mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka Kundi la Weusi, Nikki wa Pili amesema wameamua kuidhamini michuano hiyo kutokana na kuwavutia watu wa kipato cha kati na cha chini ambao ambao wanaendana na huduma za kibenki wanazotoa.

Nikki alisema benki hiyo inawahudumia hata wateja wenye kipato kidogo kabisa ambapo alisema wanaweza kufungua akaunti kwa Shilingi 5000/=.

Katika funguzi huo timu za Mabibo Market na Keko Fenicha zilioneshana umwamba ambapo mpaka mwisho wa mchezo Mabibo Market ilichapa Keko Fenicha kwa mabao 3-2.

Katika uzinduzi huo kama kawaida ya michuano hiyo vituko vilitawala mwanzo mwisho.



Shabiki wa Keko Fenicha akiwa amejipaka rangi mwilini. 
Wachezaji wa Mabibo Market wakishangilia bao la pili.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/GPL