
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameendesha zoezi la kuosha magari ya wabunge ili kuhamasisha uchangiaji wa fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 3 zitakazosaidia kujenga vyoo kwa matumizi ya watoto wa kike wenye mahitaji maalum nchini.

Shughuli hiyo imefanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma na kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 17.2.
