
Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo na Star Times jana wamezindua huduma Star Times App ambayo itawawezesha watumiaji wa simu za Smart Phone kujionea kombe la dunia laivu kupitia simu zao.

Akizungumza na wanahabari kwenye mkutano uliofanyika Hoteli ya Slipway Jijini Dar jana, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema katika mchakato huo wao watatoa internet katika kuwezesha mchakato huo na Star Times ndiyo wenye App hiyo.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Matangazo wa Star Times, David Malisa amewataka watumiaji wa mtandao wa tigo kupakua App hiyo ili kujionea matukio muhimu ya kombe la dunia ambapo watumiaji hao wataweza kurekodi mechi wanayoitaka kwa ajili ya kuitazama vizuri watakapopata muda muafaka.



HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL