×

Huddah Awashangaza Mashabiki wa Dar Live

Mrembo na Mwanamitindo kutoka nchini Kenya Huddah ‘The Boss Chick’ akiwasalimia mashabiki baada ya kupanda stejini kama ‘special host’ wa ‘Usiku wa Kusi’.
…Akiwapongeza mashabiki kwa kufika kwenye shoo hiyo.
…Akionyesha ‘machejo’ ya kulishambulia jukwaa.
…Akitambulisha bidhaa zake za vipodozi kwa kutoa zawadi kwa wasichana kumi aliowaita stejini.
Mashabiki wakiendelea kupata zawadi.

MREMBO na mwanamitindo kutoka Kenya, Huddah, maarufu kama The Boss Chick, usiku wa kuamkia leo alipanda katika steji ya ‘Usiku wa Kusi’  katika Ukumbi wa |Taifa wa Burudani wa Dar Live kwa kucheza wimbo wa African Beauty wa Diamond Platinumz huku mashabiki wakimshangilia kwa kuvutia na mwonekano wake na uchezaji wake.

Pia alitumia fursa hiyo kuzindua bidhaa zake za vipodozi kwa kuwagawia kina dada kumi miongoni mwa wengi waliofika katika shoo hiyo.

PICHA NA RICHARD BUKOS/MUSA MATEJA