
KAMPUNI ya simu ya Infinix kuzindua simu mpya ikiwa ni muendelezo wa Infinix NOTE 4 kwa kushirikiana na GOOGLE.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Juni mwaka huu Barani Afrika Nchini Dubai katika jengo la Burj Khalifa.
Kwa pamoja ikishirikiana na GOOGLE kampuni ya simu ya Infinix imeweka nia ya kuzindua simu iliyo na ubora zaidi ya matarajio ya wengi na inasemekana kupitia ushirika wake na GOOGLE ujio wa simu zote za NOTE kutumia mfumo wa Android 1 (A1) wenye ufanisi zaidi ya Android Oreo.
Zaidi ya watu 200 mpaka sasa wameshapata mwaliko kutoka katika kampuni hizo mbili kwenda kushuhudia uzinduzi huo pamoja na kushuhudia namna Android 1 (A1) inavyofanya kazi kupitia GOOGLE Assistant na GOOGLE Lens.
Akizungumzia mafanikio ya kampuni hiyo, Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo ya Infinix , Erick Mkomoye alisema kwamba, tangu kutambulishwa kwa kampuni ya Infinix mwaka 2013, kampuni imeweza kudhihirisha ubora wake na kuweza kupenya katika masoko ya Afrika na wako mbioni kuwaletea wateja wao teknolojia mpya kupitia simu mpya itakayozinduliwa wiki ijayo.